MAAFISA UNUNUZI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ILI KUBORESHA HUDUMA
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndugu Kusirie Swai amewataka Wakuu wa Vitengo na Ununuzi kwa Umma na Mipango kutumia vyema sheria za Ununuzi kwa umma, Ubia kwa sekta binafsi na umma na takwimu katika kuboresha huduma kwa jamii.
Ndugu Swai Ametoa wito huo leo Septemba 6, 2024 wakati akifungua mkutano wa kikanda kuhusu sheria ya ununuzi wa umma, ubia kati ya sekta ya umma na binafsi na matumizi ya twakwimu zinazowasilishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Ndugu Swai amesema mipango ya Serikali katika kuhudumia wananchi imewekewa sheria ili kuhakikisha wanaotekeleza majukumu hayo wanazifuata ili kuhakikisha kunakua na ufanisi na hatimaye kuleta matunda chanya kwa jamii hivyo ni wajibu wao kuzingatia weledi.
"Ndugu washiriki, mpo hapa ili kujifunza mapya na kukumbushwa taratibu zinazopaswa katika kazi zenu ili tukasaidie juhudi za Serikali katika kuboresha huduma kwa hiyo naomba mzingatie maelekezo mtakayopewa." Ndugu Swai.
Awali, Afisa Sheria Mkuu Idara ya sheria kutoka Wizara ya Fedha Ndugu Paul Kimweri amefafanua kuwa wizara hiyo imeandaa mafunzo hayo ili kutoa ufahamu kwa Maafisa Ununuzi na Mipango juu ya sheria ya ununuzi wa umma ya 2023, sheria ya ubia ya sekta ya umma na binafsi na matumizi sahihi ya Takwimu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.