Usalama wa mipaka ,kulinda mali za raia na kufuata sheria ndiyo msingi wa kuleta maendeleo katika ukanda wa Ziwa.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella alipokuwa wakiwaeleza Maafisa Wakuu kutoka Chuo Cha Ukamanda na Unadhimu kilichopo eneo la Duluti, Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha historia ya Mkoa wa Mwanza na shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanyika na kulifanya jiji hilo kukua kwa kasi na kuchangia asilimia 32.4 la pato la taifa.
Alisema wanafursa mbalimbali za kiuchumi huku wao wakiwa wamewekeza katika sekta ya Uvuvi, kilimo, biashara na viwanda pia usafirishaji wa samaki kwenda ulaya ni fursa kubwa inayochochea kukuza uchumi wa wakazi na taifa.
Brigadia Jenerali Sylvester Ghuliku Mkuu wa chuo cha Ukamanda na Unadhimu Duluti Arusha anasema wanatoa mafunzo kuanzia cheo cha Meja na kuendelea ili kuwajengea waweza kukabiliana na matatizo mbalimbali ya utendaji pia chuo hicho kinanachukua wanafunzi kutoka ndani na nje ya nchi .
Anasema katika awamu hii wanawanafunzi 65 amboa wamegawanyika katika makundi mawili ,moja likiwa Dar es salaam na lingine Mwanza lengo likiwa baada ya mafunzo ya darasani wanatoka nje kwenye maeneo ya wananchi kwa ajili ya kufanya utafiti na kuona vitu vinavyoendelea katika shughuli za uraiani.
" Timu yetu ilikuwa ya kufanya tafiti ya uongozi na maendeleo tumechagua Jiji la Mwanza baada ya kuona kuna miradi mingi ya kimkakati inayofanywa na serikali hivyo tulitaka kujifunza kuona na kujadili na viongozi watendaji kwenye hiyo miradi baada ya kufanya ziara tumekuja kushuhudia tukio la kuingizwa majini kwa Mv. Ukara ll kwani ni shughuli ya kimaendeleo kwa ajili wananchi wetu , utafiti wetu kuhusu uongozi na maendeleo kwa mkoa huu" anaeleza Ghuliku.
Washiriki 32 ndiyo waliowasili Mkoani hapa kwa Ziara ya mafunzo ambapo chuo hicho kinasimamiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na wanachuo hao wanatoka Tanzania, Burundi, Kenya, Uganda na Zibambwe.
Aidha,Maofisa kwa pamoja wamepata fursa ya kutembelea Songoro Marine na kujionea majaribio ya Kwanza kuingiza ziwani kivuko Cha MV. UKARA II Hapa kazi Tu kilichotengenezwa na Kampani ya Songoro Marine kwa gharama ya Shilingi Bilioni 4.2 ikiwa ni Fedha za Serikali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.