MABORESHO YA KITUO CHA AFYA MKOLANI YAONGEZA HUDUMA KWA WAKAZI 14,000
Maboresho ya kituo cha afya Mkolani yaliyo gharimu shs milioni 848 kimesaidia kuongeza huduma bora kwa wananchi kutoka kata 10 na kufikia idadi ya 14,000 wanaofika kupata matibabu.
Mganga Mkuu wa kituo hicho Leonard Kafula akitoa leo taarifa fupi kwa Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza Balandya Elikana,amesema awali kabla ya maboresho walikuwa wanatoa huduma kwa wateja wapatao 15 hadi 20 lakini sasa hivi wanawahudumia 70
Amesema maboresho hayo ya miundombinu yaliyoanza kufanyika mwaka 2022-23 kwa mfumo wa force account ,Serikali kuu imetoa shs milioni 248,imetoa pia shs milioni 300 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba na shs milioni 300 zimetolewa na halmashauri ya Jiji la Mwanza kupitia mapato yake ya ndani.
"Kukamilika kwa mradi huu kumeboresha na kuwezesha kupatikana kwa huduma zote ikiwemo ya upasuaji huku idadi ya akina mama wajawazito ikiongezeka kutoka 15 hadi kufikia 37 kwa mwezi na kupunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa kwenda kupata huduma hiyo hospitali ya Nyamagana.
"Ndugu Katibu Tawala wetu kituo hiki sasa kimekuwa mkombozi kwa wananchi wa Mkolani na maeneo ya jirani lakini hasa wakina mama wajawazito ambao walikuwa wakilazimika kwenda umbali mrefu kupatiwa huduma na wakati mwingine kuhatarisha uhai wao,"Mkuu wa wilaya.
Mara baada ya kukagua kituo hicho Ndugu Balandya amewataka watumishi kuwahudumia wateja wao kwa weledi licha ya kuwepo kwa changamoto ya upungufu wa watumishi hali ambayo inafanyiwa kazi na Serikali kulingana na bajeti.
Miradi yenye thamani ya zaidi ya shs bilioni 78 wilayani Nyamagana imefanyiwa ukaguzi ikiwemo ya maji,shule na barabara.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.