Kambi ya Madaktari Bingwa yaanza kwenye Viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure kwa kushirikiana na Hospitali ya Bugando ambapo wananchi watafanyiwa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali kwa siku tano.
Akizindua kambia hiyo mapema wiki hii, Katibu Tawala wa Mfkoa wa Mwanza Ndugu Balandya Elikana ametoa wito kwa wananchi wa Mwanza na maeneo ya jirani kufika kwenye viwanja hivyo kufanya vipimo ili wafahamu afya zao na kuweza kupata tiba.
"Nawakaribisha sana wananchi kwenye viwanja hivi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni kwa siku tano mfululizo ambapo pamoja na kupata uchunguzi wa magonjwa mbalimbali, kutakuwa pia na vipimo kama vya Selimundu, Kansa ya Damu, Mionzi, Upungufu wa Damu Mwilini na vingine." Elikana.
Naye, Daktari Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Bahati Msaki amesema Afya ndio mtaji wa maisha ya kila mwanajamii hivyo ni wajibu wa wananchi kutumia fursa hiyo kupata vipimo huku akibainisha kuwa wanatarajia kuhudumia zaidi ya wananchi 2000 kwenye kambi hiyo.
"Kuna Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Macho, Meno, Watoto, Magonjwa ya akina mama na watoto, Magonjwa ya damu, Mfumo wa Chakula, Magonjwa ya Akili, huduma za kusafisha Damu, Maabara na Damu." Amesisitiza Dkt. Bahati Msaki.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.