MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA
Itakumbukwa mnamo machi 16 na machi 26, 2025 Makundi mawili ya Watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza walikwenda kufanya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Ngorongoro, Hifadhi ya Taifa ya Mwl. Nyerere, Mradi wa kimkakati wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) na Mradi wa reli ya kisasa kutoka Mkoa wa Dar es Salaam kwenda Dodoma.
Leo Aprili 29, 2025 makundi hayo mawili kwa uwakilishi yamewasilisha neno la shukrani na zawadi kadhaa Ofisini kwa Mratibu na Muasisi wa Ziara hizo ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana.
Akizungumza ofisini kwa Katibu Tawala, Kiongozi wa Kundi la JNHPP Bw. Paulo Cheyo amesema ilikua ni wasaa mzuri sana kutembelea mradi wa kimkakati wa JNHPP na wameweza kujifunza mengi na kumtakia kila la kheri KIongozi huyo mwenye maono mema kwa Watumishi wake.
“Hakika safari yetu ilikua nzuri na yenye mafunzo, Binafsi sikuwahi kufikiria kufika kutazama uwekezaji mkubwa uliofanywa katika bwawa la Mwl. Nyerere, Ninakushuru sana Kiongozi kwa jitihada zako”. Amesema Bw. Mangabe Mnilago.
Naye Kiongozi wa Kundi la Ngorongoro - Serengeti Bw. Credo Lugaila amesema ziara hizo pia zimesaidia kuwachangamsha na kuleta ari ya ufanyaji kazi, lakini pia amesema imesaidia kuimarisha mahusiano mazuri baina ya Watumishi na Viongozi wa Mkoa.
“Maneno Matakatifu ya Biblia yanasema upendo wa ndugu na udumu, Tunakushuru sana Baba kwa upendo wako, umethibitisha maana halisi ya Kiongozi anaejali na kuwathamini Watumishi wake, Tunakushuru sana. Amesema Bi. Ine Sibale
Akihitimisha kutoa shukrani hizo Bi. Zawadi Kalilo amesema upendo wa Katibu Tawala ni kama upendo wa Baba lakini kwa Kiongozi huyo kwa Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amekuwa kama “Daddy”. (Akimaanisha mwenye upendo uliokithiri).
Akizungumza mara baada ya kupokea salamu hizo, Katibu Tawala Bw. Balandya Elikana amewashukuru kwa maneno mazuri ya faraja pamoja na maombi na amewataka sasa kwenda kuchapa kazi kwa ufanisi na weledi.
Makundi hayo mawili yamewawakilisha wale Watumishi waliopata wasaa wa kufanya utalii na wamemzawadia kiongozi huyo zawadi mbalimbali ikiwa ni kitambua mchango wake katika kuwathamini Watumishi hao na kwake ikawe kumbukumbu halisi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.