MAKUZI YA AWALI YA MTOTO MSINGI WA UJENZI WA TAIFA IMARA - RAS BALANDYA
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana amesema ili kujenga familia imara na taifa lenye nguvu ni muhimu kuwalea watoto katika mazingira mazuri yatakayo wawezesha kutambua fursa zilizopo hatimaye kujiletea maendeleo katika ngazi ya familia na Taifa kwa ujumla
Akizungumza leo Mei 16, 2025 katika kikao cha taarifa ya utekelezaji wa programu jumuishi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto mkoa wa Mwanza robo ya tatu Januari Machi, 2025 Bw. Balandya amesema msingi wa maisha bora itategemea namna watoto watakavyokuwa wamelelewa.
Kadhalika, Bw. Balandya amesisitiza kuwa ili mtoto aweze kufikia hatua zote za ukuaji ni lazima alindwe na kulelewa katika mazingira salama na afya bora hatimaye hapo baadae awe mwenye uwezo wa kukabiliana na changamoto zote zitakazomzunguka.
“Japo kuna baadhi ya jamii zinachukulia jambo hili kwa uzito mdogo lakini ndio lenye matokeo makubwa katika kuimarisha uwezo wa binadamu kufanya vizuri kielimu na maisha ya kijamii ikiwemo kuwa na maisha bora”. Amesema, Balandya.
"Na sisi wazazi kwa pamoja na wataalamu ndio tumebeba jukumu na dhamira ya kuhakikisha hilo linatokea na ni lazima tufanye vizuri katika kutekeleza majukumu yetu." Ameongeza Katibu Tawala Mkoa.
Aidha, Katibu Tawala amesema mkoa wa Mwanza kupitia halmashauri zake 8 wanazo timu ya zinazofanya ufuatiliaji kila siku wa utoaji za huduma kwa watoto popote walipo, timu hizo zinajumuisha wtaalamu wa elimu, afya, ustawi wa jamii, maendeleo ya jamii na jeshi la polisi kupitia dawati la jinsia.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.