Leo Januari 13, 2025 Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSF) Kanda ya Ziwa Bw. Rajabu Kinande amewasilisha salamu za Sikukuu za Mwaka Mpya kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bw. Balandya Elikana.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo iliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Meneja wa PSSF alisema lengo la kufika ni kuwatakia viongozi hao heri ya mwaka mpya wa 2026 pamoja na kuendelea kuimarisha mahusiano ya kikazi kati ya PSSF na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya ustawi wa watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameishukuru PSSF kwa salamu hizo na kwa ushirikiano mzuri unaoendelea kati ya taasisi hiyo na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.