Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amewataka watumishi wa ardhi Mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanatenga siku kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi zinazohusiana na ardhi.
Akiongea katika Mkutano uliofanyika katika viwanja vya ukumbi wa Gandhi Hall Wilaya ya Nyamagana Mhe. Mongella amesema watumishi wajikite katika kutatua migogoro ya wanannchi na si kuiahirisha kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza kiasi kikubwa cha migogoro ya ardhi Mkoani Mwanza.
Aidha amesisitiza kuwa Maafisa ardhi watumie taaluma yao kutatua matatizo ya wananchi wenye migogoro ya ardhi, na ifike sehemu mtu mwenye mgogoro akienda idara ya ardhi arudi ameridhika na majibu aliyopewa na siyo kuongezeka kwa tatizo kutokana na kuahirisha tatizo hilo.
Hata hivyo ameongeza kuwa wingi wa watumishi katika Jiji la Mwanza uwe suluhisho la kutatua migogoro kwa haraka na ifike wakati matatizo yamalizike na siyo kila mwezi kushughulikia matatizo yaleyale bila kuyapatia ufumbuzi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.