Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella ameweka jiwe la msingi Kituo cha Afya cha Kamanga kilichojengwa kwa ushirikiano baina ya Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Shirika lisilo la Serikali lijulikanalo kama CEDAR FOUNDATION lenye Makao Makuu yake Nchini Uswisi kwa Tanzania lina Ofisi yake Jijini Mwanza.
Ujenzi wa Kituo hicho ulianza Februari 2015 na kumalizika Novemba 2017 ambapo ujenzi huu unafanyika kwa awamu, na kwa sasa limejengwa jingo la wagonjwa wan je lenye vyumba 23 na nyumba 9 za watumishi,hadi kukamilisha Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ilichangia Jumla ya Shilingi 59,126,098.50 ambapo kati ya hizo 52,693,000 zilitumika kutengeneza mfumo wa maji na Shilingi 3,800,000 ziliweka mfumo wa umeme wakati 1,433,097.50 zilitumika kulipia hati miliki ya eneo na Shilingi 1,200,000 zilitumika kupima eneo la kituo.
Shirika la CEDAR FOUNDATION limechangia jumla ya Shilingi bilioni 2.325 ambapo fidia kwa waliokuwa wakazi wa eneo hilo ni shilingi milioni 251, ujenzi ni shilingi bilioni 1.55, tofauti na ujenzi Shirika limetoa vifaa tiba vyenye thamani ya ya Shilingi milioni 331 ikiwa ni gharama ya vifaa hivyo na usafirishaji,pia imegharamia vifaa vya ofisi kama jenereta,mashine ya kuchomea taka hatarishi na kufunga mfumo wa kielektroniki kwa thamani ya shilingi milioni 193.
Mhe.Mongella awali akiwapongeza wafadhili hao amesema kuwa, Mradi huu unategemea kutoa huduma bora za afya na ustawi wa wananchi zaidi ya watu elfu 30 wa kata ya Nyamatongo na kata nyingine za jirani, hivyo utasaidia vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema.
Mhe. Mongella ameongeza kuwa, pamoja na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali pamoja na wadau wa maendeleo Ikiwemo CEDER FOUNDATION, Sekta ya Afya Mkoa wa Mwanza inakabiliwa na changamoto mbalimabli ikiwa ni pamoja na upungufu wa watumishi wa afya kwa asilimia 51,ukowefu wa vituo vya huduma katika vijiji 303 na uwepo wa majengo ambayo hayajakamilika 109 katika vijiji na baadhi ya ya vituo vya huduma, upungufu wa nyumba za watumishi wa afya 951,ukosefu wa mashine muhimu za uchunguzi katika Mkoa(MRI), mwitikio mdogo wa jamii kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF ambapo kwa sasa ni 10.89% ya waliojiunga na o.71%(TIKA) lengo likiwa ni asilimia 30.
Hata hivyo, katika kukabiliana na changamoto hizi Mkoa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo unaendelea kuboresha miundombinu ya utoaji huduma za afya, ununuzi wa vifaa muhimu vya uchunguzi wa magonjwa, ufungaji wa mifumo ya kielektroniki katika vituo vyote vyenye umeme na kutenga nafasi za ajira kila mwaka.
Aidha, Mkoa umepokea Bilioni 2.62 kwa ajili ya upanuzi wa vituo vya afya Mkoani Mwanza hivyo utahusisha ujenzi wa majengo ya huduma za upasuaji wa dharura za uzazi, wodi za wazazi, maabara na nyumba za watumishi utakaotekelezwa katika vituo 6 vya afya, ambapo ujenzi wa awamu ya kwanza umeanza katika vituo viwili vya Kahangara –Magu na Karume – Ilemela na awamu ya pili itahusisha vituo vya Afya vya Bwisya – Ukerewe na Malya – Kwimba, Kome- Buchosa na Kagunga – Sengerema.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.