MHE. MTANDA ATAKA MABORESHO UTEKELEZAJI MKATABA WA LISHE
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka watendaji kutoka idara ya afya kufanya vikao na makundi mbalimbali kwenye vijiji ili kutoa elimu kwa jamii dhidi ya masuala ya lishe ili wananchi wapate uelewa na kuweza kushiriki katika kujenga jamii yenye afya bora.
Mhe. Mtanda ametoa agizo hilo mapema leo agosti 27, 2024 wakati akifungua kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe kuanzia Julai 2023 hadi Juni 2024 baada ya kubaini kuwa watendaji katika sekta husika wamekua nyuma kwenye kutekeleza afua.
"Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na wadau tutaendelea kutekeleza afua za lishe ili kutekeleza mkataba wa lishe na kuleta tija kwa jamii ya Mwanza na Taifa kwa ujumla".
Aidha amesema upangaji na utoaji wa fedha umeimarika kwa halmashauri kwa zaidi ya 92% na zaidi ya watoto laki moja wamepatiwa matone ya vitamini A.
Sambamba na hayo pia Mkuu wa Mkoa ametoa onyo kwa halmashauri ya Jiji la Mwanza kuacha tabia ya kutumia fedha za usimamizi wa utekelezaji wa afua za lishe katika vituo vya kutolea huduma za afya na kwa watoa huduma ngazi za jamii kwa shughuli zingine kwani wanakwamisha mkataba wa lishe wa mkoa.
Kadhalika, amezitaka Halmashauri za Ukerewe na Misungwi kuongeza nguvu kwenye utoaji fedha katika shule kwa ajili ya shughuli za lishe na amewapongeza Manispaa ya Ilemela kwa kutoa zaidi ya asilimia 97 ya fedha walizojipangia na katika kusimamia hilo amewataka waratibu kuwashirikisha wakuu wao wa Wilaya mara kwa mara ili kuwajengea uelewa.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa afua za lishe Mratibu wa Lishe Mkoa wa Mwanza Bi. Sophia Lugome amesema Mwanza ina ukondefu kwa watoto kwa chini ya 5% na ametoa wito kwa wamama kunyonyesha watoto kwa miezi 6 bila kuwapa chakula chochocte na amewataka kuwapeleka hospitali watoto wenye utapiamlo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.