MICHEZO INA NAFASI KUBWA YA KUTANGAZA UTALII :RC MTANDA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda ameshiriki mbio za kuhamasisha Utalii mkoani humo maarufu kama Transec Lake Victoria Marathon na kusisitiza michezo ni njia muhimu ya kutangaza na kukuza utalii ikiwemo na vyakula vya kitamaduni.
Akizungumza leo Julai 7,2024 kwenye uwanja wa Nyamagana mara baada ya kuhitimishwa Marathon hiyo ambayo naye ameshiriki,amebainisha Mwanza una vivutio vingi vya utalii hivyo juhudi inayotakiwa sasa ni Jamii kuvitangaza ili viweze kujulikana ndani na nje ya nchi
Aidha amewapongeza waandaaji wa mbio hizo kwa ubunifu huo unaohitaji kuigwa pia wakimbiaji wote wa walioshiriki kilomita tofauti kama km 21,km10,km 5, na km 2 na washindi kupata nishani na zawadi ya pesa zilizotolewa.
"Sekta ya utalii inachangia pato la Taifa kwa asilimia 17 kwenye GDP ya nchi vivyo hivyo inatoa ajira kwa watanzania zaidi ya milioni 1.6 hivyo ni sekta muhimu kwa Taifa letu",Mkuu wa Mkoa.
Naye Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza Sunday Peter amewashukuru wakimbiaji kwa kuwa na nidhamu na kufuata maelekezo wakati wa mbio hizo na kuwezesha kikosi cha usalama barabarani kufanya kazi yao kwa wepesi .
Kwa upande wake Rais wa Chama cha Riadha Tanzania Silas Wambura amesema ametoa wito kwa wanamichezo kushiriki mbio mbalimbali zinazoandaliwa nchini ili kuwapata washiriki bora watakao iwakilisha Tanzania katika medani kimataifa.
Mbio hizo zilikuwa na lengo la kuhamasisha utalii wa ndani kanda ya ziwa pamoja na kuchangia taulo za kike kwa wasichana.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.