Kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Ziwa Magharibi kimefanyika katika Ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa,Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza Christopher Kadio amesisitiza Halmashauri zote za kanda ya ziwa magharibi kushiriki kikamilifu katika Maonyesho ya mwaka huu na kuwataka washiriki wa kikao kutoa mawazo ya kuboresha maonyesho ya mwaka huu.
Aidha amezitaka Halmashauri zinazodaiwa michango ya maandalizi ya shughuli za nanenane kumalizia michango hiyo kwa wakati.
Awali akiwasilisha mada ya mapato na matumizi ya maadhimisho ya nane nane Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Emil Kasagala amesema kiasi cha Shilingi 120,939,400 zimekisiwa kutumika kufanikisha maadhimisho ya mwaka huu kwa kanda ya Ziwa Magharibi.
Akichangia kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Josephat Maganga aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Geita amesisitiza mshikamano na ushirikiano miongoni mwa Halmashauri na Mikoa shiriki kama nguzo muhimu ya mafanikio ya maadhimisho haya ya Nane nane 2019.
Akihitimisha kikao hicho Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Christopher Kadio amewashukuru wajumbe wote waliohudhuria na kusema kuwa mambo mazuri hufanywa na watu wachache ila yakifanikiwa wanakuwa wengi zaidi hana wasiwasi na uchache wa wajumbe na kuonyesha imani kubwa ya mafanikio.
Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Geita ameahirisha kikao kwa kuwashukuru washiriki wote kwa usikivu,utulivu na hasa kwa mawazo ya michango na kusema kuwa anaamini mawazo yote yatarejea katika Halmashauri zote na kufanyiwa kazi kama maekezo yalivyotolewa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.