Mikakati ya mkoa kuudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu inaendelea: Dkt. Rutachunzibwa
Leo Januari 15, 2024 Mganga mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Thomas Rutachunzibwa ameendelea na vikao kwenye ukumbi wa Ofisi yake na kamati za kisekta za Mkoa za kuudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu.
Kamati hizo zinazoundwa na wajumbe kutoka Wizara ya afya na taasisi mbalimbali yakiweno mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayotoa huduma za afya,vikao hivyo vya kila siku wanajadiliana majukumu mbalimbali wanayopeana ya kupambana na ugonjwa huo kwenye Wilaya za Nyamagana na Ilemela.
Akizungumzia mikakati hiyo Dkt. Ruta amebainisha wajumbe hao wanakutana mara mbili kwa siku asubuhi kupeana taarifa za nini cha kufanya siku husika na jioni kupata mrejesho na changamoto za kufanyiwa kazi kwenye kwenye maeneo yote husika.
"Tumeunda Sekta za kimkakati mfano tuna MWAUWASA,RUWASA na Maabara ya maji majukumu yao ni kuhakikisha vyanzo vyote vya maji vinatambuliwa na kutibiwa,kupima ubora wa maji yanayotumiwa na wananchi kupitia mifumo rasmi na isiyo rasmi,"amefafanua mganga mkuu wa mkoa.
Amesema sekta ya elimu kwa kushirikiana na sekta ya afya watafanya ukaguzi wa vyoo vinavyotumika na walimu pamoja na wanafunzi,kuzuia uuzaji holela wa vyakula na matunda shuleni na uwepo wa sehemu maalum za kunawa mikono zenye maji tiririka na sabuni.
"Sekta ya Tarura na Tanroad watakuwa na jukumu la kufanya ukaguzi wa mitaro yote ya barabarani ili kuepusha takataka kusambaa maeneo yasiyo husika na kuhakikisha barabara zote zinapitika ili kurahisisha usafirishaji wa wagonjwa kwa urahisi huku sekta ya viongozi wa dini wanatakiwa kutoa elimu kwa waumini wao na kuwa na vyoo bora na kutumika,"Dkt.Rutta.
Dkt.Ruta ambaye ni Mwenyekiti wa kamati hiyo mkoa amesema sekta ya wataalamu wa afya,Ustawi wa jamii na Lishe wanatakiwa kuandaa kambi za matibabu ya wagonjwa,na kuhakikisha kila halmashauri ina mahitaji yote muhimu kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.