*Mkoa wa Mwanza wazindua rasmi mfumo wa m-mama kwa wajawazito,waliojifungua na watoto wachanga*
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg.Balandya Elikana amezindua rasmi mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa wakina mama wajawazito,waliojifungua na watoto wachanga(m-mama) na kuwataka wahusika wote na mfumo huo kutekeleza wajibu wao kwa weledi.
Akizungumza na wafanyakazi wa kitengo hicho leo kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza,Seko Toure,Balandya amesema lengo la kuanzishwa kwa mfumo huo ni kuepuka vifo vya mama na mtoto ambapo Mkoa wa Mwanza unakabiliwa na Changamoto hiyo,hivyo haitakuwa na maana kama wahusika wataonesha kuzembea katika kuteleza wajibu wao ipasavyo.
"Serikali ya Rais wetu Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan imeipa kipaumbele Sekta ya afya kwa kuboresha maeneo mbalimbali likiwemo hili la mfumo ambao ulizinduliwa na Rais wetu," amesema Mtendaji huyo wa Mkoa.
Ameongeza kuwa wahusika wote wa kada ya afya sasa watambue ni wajibu wao kuja na matokeo yenye tija wakati Serikali ikiweka mikakati mbalimbali ya kuwaboreshea huduma wananchi wake.
"
Mimi nikiwa Muuguzi Mkuu wa Mkoa,nimeguswa kwa namna ya pekee na huduma hii kwani ni yenye nia njema kwa wakina mama na watoto na hasa kwa wale walio katika maeneo yenye changamoto ya umbali na usafiri," Bi.Claudia Kaluli,Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa.
Afisa mwandamizi wa TEHAMA kutoka Wizara ya Afya,Jackson Shayo amesema mfumo huu umeonesha kuitikiwa vyema Bara na Visiwani hali ambayo inaonesha ni mkombozi kwa wakina mama wajawazito na wototo.
Huduma hiyo ya m-mama imefanikishwa na baadhi ya marafiki wa Maendeleo ikiwemo Vodafone Foundation,Pathfinder International na Touch Foundation
Jumla ya madereva 114 wameingia mkataba wa kutoa huduma hiyo katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Mwanza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.