Wananchi wa kisiwa cha Kweru mto ndogo kilichopo wilayani Ukerewe wamelazimika kujenga shule ya msingi ili kunusuru maisha ya watoto wao waliokuwa wakilazimika kuvuka maji kwenda ng’ambo ya pili kuifuata elimu kwa kutumia mitumbwi.
Akizungumza wakati wa ziara Mkuu wa wilaya hiyo Mhe.Cornel Magembe alisema Shule ya Msingi Shikizi ilijengwa kwa usimamizi wa polisi hiyo, ni baada ya kuibuka kundi la watu wakidai eneo hilo kuna makabuli ya babu zao lengo likiwa ni kukwamisha harakati za ujenzi wa shule hiyo.
Alisema kipindi cha nyuma watoto walilazimika kupanda mitubwi kuifuata elimu kisiwa jirani jambo ambalo lilisababisha watoto kupata adha mbalimbali hivyo wananchi waliungana na kuweza kujenga vyumba vinne vya madarasa,ofisi moja na matundu ya choo mawili.
“Shule hii ni mradi uliogharimu Tsh 33,000,000/- ambapo inahusisha mchango wa Mkurugenzi, Mchango wa wananchi pamoja, NMB na mifuko 193 ya saruji fedha za Mfuko wa jimbo, katika kisiwa hicho”alisema Mhe.Magembe.
Awali mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ambaye ni diwani kata ya Kanguli George Nyamaha amemweleza adhima ya wananchi wa kisiwa hiko kuwa ni kuboresha elimu na wapo tayari kukamilisha ujenzi kwa mifuko 193 iliyotolewa na Mbunge ili kupatiwa usajili hivyo wananchi wa kisiwa hicho walilazimika ujenzi wa shule kutokana na changamoto hiyo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella aliwapongeza kwa maendeleo hayo kwani kuna maeneo ambayo yanawakazi wengi lakini hawana hamasa ya kujenga shule hivyo alimuagiza Afisa Elimu wa Mkoa Michael Ligola kualakisha usajili wa shule hiyo ili kuwanusuru na adha hiyo, na kuahidi kuchangia bati mia moja ili kuunga mkono juhudi za wananchi hao.
“Kuna maeneo watu ni wengi na wanashindwa ata kujenga shule, ujenzi kwao ni ugomvi na mabishano wananchi wote wangekuwa kama wakazi wa kisiwa hiki tungekuwa mbali sana kimaendeleo na nitafuatilia madarasa mawili yaliyosalia pamoja na ujenzi wa Choo ili shule hiyo ipatiwe usajili kamili.”alisema Mhe.Mongella.
Naye Afisa Elimu Mkoa Michael Ligola alisema Shule hiyo inatakiwa kusajiliwa ili kuwanusuru watoto hao hivyo wajitahidi kumalizia madarasa mawili na matundu ya vyoo ili kukudhi vigezo baada ya hapo watawapitisha wakaguzi na shule hiyo itasajiliwa.
Aidha wananchi wa eneo hilo wakizungumza katika mkutano wa hadhara Frank Vicent na Yusta John walisema baada ya watoto kushindwa kwenda shule unapovuma upepo ziwani wamechukua hatua hiyo ambapo hatua ya kwanza walianza na ujenzi wa shule kwa kutumia mabanzi ,wanafunzi walisoma hadi pale walipojenga shule hiyo pia waliiomba serikali kusaidia kumaliza mapungufu yaliopo ikiwa pamoja na usajili wa shule hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.