Bohari kuu ya dawa nchini-MSD imeshauriwa kuharakisha zoezi la kusambaza vifaa tiba katika kituo cha afya cha kagunga wilayani sengerema mkoani mwanza ili kuwezesha zaidi ya wakazi elfu hamsini wa kata za kagunga,igalula pamoja na maeneo jirani kupata huduma za afya.
Wito huo umetolewa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Charles Kabeho wakati akiweka jiwe la msingi la msingi la ujenzi wa majengo matano ya kituo cha afya cha kagunga ambao umeigharimu serikali shilingi millioni 402.
"MSD yawezekana wana ratiba zao za kutoa bifaa tiba lakini mimi niwaombe pale vituo vya afya na hospitali zinapokamilika waharakishe kupeleka vifaa hivyo ili kuharakisha husuma kwa wananchi," alisema Kabeho.
Serikali baada ya kukamilisha ujenzi wa majengo matano ya kituo cha afya Kagunga wilayani sengerema mkoani mwanza ikiwemo jengo la upasuaji,wodi ya wazazi na maabara,majengo hayo yanategemea kukuanza kuta huduma kwa wananchi wa maeneo hayo lakini bado huduma hazijaanza.
Hali hiyo imebainika wakati wa mbio za mwenge wa uhuru na hivyo kumlazimu kiongozi wa mbio huyo kutoa rai kwa bohari kuu ya dawa nchini.
Kiongozi huyo pia ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Nkumba wilayani Sengerema na kuitaka jamii kuchangia maendeleo ya elimu ili kutatua changamoto zilizopo.
Katika kijiji cha Nyamasale zaidi ya wananchi elfu mbili wa kijiji hicho wameondokana na tatizo la maji baada ya mwenge wa uhuru kuzindua kisima kirefu cha maji kilichogharimu shilingi millioni 26.
Aidha, Mwenge wa uhuru ukiwa wilayani Sengerema umezindua,kukagua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mitano ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi billioni moja,miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa barabara ya bomani yenye urefu wa kilometa 0.4 kwa kiwango cha lami.pamoja na ghala la kuhifadhia mazao katika kijiji cha Isole limegharimu millioni 365.
Aidha,amezindua ghala la kuhifadhia mazao katika kijiji cha Isole lenye gharama ya Shilingi Milioni 365.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.