Zoezi la uandikishaji wananchi kwenye daftari la Mkazi mkoani Mwanza kwa ajili ya kurasimisha orodha kamili ya wapiga kura watakaoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa limeanza rasmi tarehe 8 ambapo litadumu hadi Octoba 14.
Akizungumuzia hali hiyo Msimamizi msaidizi wa kituo cha uandikishaji cha Polisi eneo la wazi mtaa wa PPF kata ya Kiseke Hellen Mcharo amesema mara nyingi watu husubiri siku zibaki chake ndiyo wajitokeze.
"Tumefungua kituo kwa wakati naona wananchi wanajitokeza wachache wachache mara nyingi huwa wanasubiri hadi siku zipungue,"alisema Mcharo.
"Kwa sababu ndiyo siku ya kwanza tunaamini kutokana na hamasa inayoendelea kutolewa basi kuanzia kesho idadi itakuwa kubwa zaidi ya leo."
"Sisi kama waandikishaji na wasimamizi tunaendelea kuwahimiza viongozi wa vyama na serikali kutoa hamasa ili kuongeza mwitikio wa wananchi kwenye zoez hili ili likamilike kwa wakati.
"Pia tunawaomba wale wananchi wachache waliojitokeza wawe kama mabalozi kwa wengine, nawaishi nao, wakazi wa Mwanza waachane na utamaduni wa kusubiri dakika za mwisho kwani tukumbuke zeozi hili ni la muda mfupi hivyo wajitokeze mapema na kwa wingi ili tumalize kujiandikisha tuanze kujiandaa na uchaguzi,"alisema Mcharo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella, amesema kuwa ili kuongeza mwamuko kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha hamasa ya matangazo inatakiwa kufanywa usiku na mchana kila mtaa ili ambaye hajapata taarifa mchana basi aipate usiku.
"Mpaka sasa zoezi bado naliona linaenda taratibu japo ndiyo tunaanza niwasihi viongozi wa vyama ma serikali tushirikiane kuongeza hamasa na wanaohusika kufanya matangazo basi wafanye hivyo hasa wakati wa usiku ili ambao hawana taarifa hizi wazipate kwa utulivu zaidi, alisema Mongella.
"Nazani hata wasimamizi mnaona wenyewe hadi sasa mmeshaandikisha wananchi ambao ni wachache sana ikilinganisha na idadi halisi ya wakazi wa mtaa huu wanaotambulika mtaani kwenu kitu ambacho kinatukumbusha kuwaamusha zaidi wasio na taarifa.
"Tuhimizane usiku kucha ili tufanikishe zoezi hili kwa maaana wapo wengine bado uelewa wao ni mpaka wapate msisitizo ndiyo wanaelewa hivyo tujitahidi twende wote tuhakikishe hakuna mwananchi anayebaki nyuma ili mwisho wa siku uchaguzi utakapofika wananchi washiriki kwa wingi," alisema Mongella.
Mmoja ya wakazi wa mtaa wa Buswelu A aliyejitambulisha kwa jina la Denis Jackson baada ya kujiandikisha ametoa wito kwa wananchi wengine kuja kwa wingi kujiandikisha kwani mbali na kuwa kufanya hivyo kunatoa haki ya msingi ya kupiga kura lakini pia zoezi la uandikishaji linakamilika ndani ya muda mfupi na halina usumbufu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.