Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amezindua Mrejesho wa Utafiti wa Vyandarua vyenye Viwatilifu vipya vya kuthibiti mbu wanaoeneza Malaria, wilayani Misungwi, unaoonesha maambukizi kushuka kutoka asilimia 51 mwaka 2018 hadi asilimia 21 sasa.
Hayo yamebainishwa Wilayani humo kupitia mradi wa utafiti wa kinga za malaria (PAMVERC) unaotekelezwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Kituo cha Mwanza, katika vijijini 72 na Kata 17 Wilayani humo.
"Nimearifiwa kuwa utafiti huu ulihusisha viwatilifu vipya aina ya Chloefenapyr ambavyo husababisha misuli ya mabawa ya mbu kukakamaa na hivyo kuzuia mbu asiruke au kutembea. Hii huzuia mbu asinyonye damu au kuruka kwenda kwa mtu mwingine, na hatimaye kufa," amesema.
Sambamba na hilo, Mhe.Mhandisi Gabriel amewataka wananchi kuendeleza tabia ya usafi na utunzaji wa mazingira kuanzia sasa mradi huo unapoelekea ukingoni, ikiwemo kufyeka majani na kuziba madimbwi ili kuua mazalia ya mbu na hatimaye kudumisha jitihada za kuzuia malaria.
Mkurugenzi wa NIMR Kituo cha Mwanza
Dkt. Safari Kinung'hi amesema mradi huo wa miaka mitano (2018-2022) umetekelezwa Misungwi baada ya kiwango cha malaria kuonekana kuwa juu.
"Malaria kwa ujumla bado ni changamoto katika Kanda yetu hii ya ziwa. Tunaendelea na tafiti ambazo matokeo yake yatatumika kuondoa tatizo hili," amesema.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.