Mwanza yapanda Miti zaidi ya Elfu 28 Kumbukizi ya kuzaliwa Rais Samia
Mkoa wa Mwanza leo Januari 27, 2024 umepanda Miti zaidi ya Elfu 28 ikiwa ni sehemu ya kusheherekea kumbukizi ya kuzaliwa ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zoezi lililoongozwa na Katibu Tawala Mkoani humo Ndg.Balandya Elikana.
Zoezi hilo la upandaji miti lililofanyika shule ya Sekondari ya wasichana ya Mkoa wa Mwanza iliyopo wilayani Magu, Balandya akiambatana na viongozi waandamizi wa Serikali wamepanda jumla ya miti 1700.
"Leo watanzania wote wanasheherekea kumbukizi ya kuzaliwa ya Rais wetu, tunapofanya jambo kama hili la kupanda miti tunaidi kuweka nchi yetu katika mazingira mazuri kwani miti ina faida nyingi," amesema Katibu Tawala wakati akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi walioshiriki zoezi hilo.
Amewataka wananchi kuendelea kuwa na tabia ya kupanda miti na kuepuka ukataji wa miti ovyo ambapo athari zake kubwa ikiwemo ukosefu wa mvua.
"Mkoa wetu tumejiwekea malengo ya kupanda miti milioni 12 kila mwaka na kila halmashauri zote 8 kupanda miti milioni 1.5 yakiwa ni maagizo ya Serikali",Balandya
"Endeleeni kuwa vinara wa kutunza mazingira kupitia elimu mnayopata hapa shuleni,muwe wana mapinduzi wa kweli katika kuifanya Tanzania kuwa ya kijani",Prof Riziki Shemdoe,Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na mifugo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.