Mwanza Yatekeleza agizo la Rais Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kwa Vitendo
Serikali Mkoani Mwanza imeanza kutekeleza agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli la kujenga jengo la abiria katika uwanja wa ndege Mkoani humo litakaloghalimu zaidi ya shilingi bilioni nne na lenye uwezo wa kuchukua abiria mia sita kwa wakati mmoja wanaoshuka kwenye ndege au wanaosubiri kusafiri.
Akikagua ujenzi wa jengo hilo katika uwanja wa ndege Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amesema ujenzi wa jengo hilo la kisasa lenye uwezo wa kuchukua abiria 600 unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 6.
"Kama mtakumbuka Mhe.Rais alipokuwa Mwanza kwa Ziara alielekeza tujenge jengo la abiria na sisi mara moja tukaanza utekelezaji wa jengo hilo kwa kuanza kazi ya kupata mchoro na sasa hivi ujenzi umeanza tupo kwenye msingi na jengo ni la kisasa na nila kudumu na kazi inaendelea vizuri,"alisema Mongella.
Kwa upande wake mbunifu majengo kutoka Ofisi Ya Katibu Tawala Mkoa Wa Mwanza Chagu Mghoma amesema Ujenzi wa Jengo hilo unaendelea vizuri huku wakiwa na wafanyakazi wa kutosha na vifaa vya kutosha Ili Kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ndani ya muda uliopangwa.
" Kazi inaendelea kama mliivyoona kila siku lazima tujiwekee malengo na lazima tuyatekeleze tuliagigwa tutekeleze kwa wakati nasi tunafuata maagizo na kazi inaendelea,"alisema Mghoma.
Naye Mtunza stoo Kopro Stephania Nasibu ameongeza kuwa wapo vizuri kuhakikisha kuwa kila kitu kinachongia na kutoka kipo katika usalama wa hali ya juu,ulinzi umeimalishwa vya kutosha.
Kwa upande wake Katibu Tawala Wa Mkoa huo Christopher Kadio amesema kukamilika kwa Jengo hilo la abiria kutasaidia kukabiliana na changamoto kubwa ya ongezeko la abiria wanaotumia usafiri wa ndege Mkoani humo.
"Ni matarajio yetu kwamba uwanja huu utakapokamilika utapunguza adha ya abiria wanayoipata pindi wanaposafiri kwani tuna taarifa kuwa uwanja huu unapokea ndege 5 zinazoenda mataifa mbalimbali kwa siku hili ni ongezeko kubwa sana," alisema Kadio.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.