Leo Agosti 25, 2025 Mwenge wa Uhuru umezindua mradi wa madarasa 11 yaliyojengwa kwa mfumo wa ghorofa katika Shule ya mchepuo wa kiingereza ya Nyanza katika mtaa wa Balewa iliyopo Halamshauri ya jiji la Mwanza huku ukigharimu fedha zaidi ya Tshs. Milioni 659.
Akiongea baada ya uzinduzi huo, kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Bw. Ismail Alli Ussi amewapongeza Wilaya ya Nyamagana kwa kutekeleza mradi wenye ubunifu uliookoa fedha zaidi ya Tshs. Milioni 132 endapo madarasa hayo yangejengwa kwa mfumo wa kawaida kwani limetumika eneo la M³ 81 pekee.
Aidha, kiongozi huyo amewasifu viongozi wa halmashauri hiyo kwa kuokoa msongamano hadi uwiano wa wanafunzi 60 kwa darasa na kwa kuongeza usajiri wa wanafunzi kutoka 110 (2022) hadi 644 (2025) jambo linaloisaidia halmashauri kupata fedha za uendeshaji hadi bilioni 3 kwa mwaka.
Bw. Ussi amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauru yaJiji la Mwanza kwa kutoa fedha za kujenga madarasa hayo kwani ameonesha utii kwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani mradi huo unasawili adhma ya kuhakikisha kuwa wanafunzi na walimu wanapata mazingira safi ya kujifunza na kufundishia.
“Ombi langu kwa vijana wa klabu ya kupambana na kuzuia rushwa tuliyoizindua leo, nendeni mkasome kwa bidii na kusimamia uadilifu na kutojihusisha na rushwa bali mkawe dira ya mapambano ya suala udhalimu huo pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya.” Amesema kiongozi huyo.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi amebainisha kuwa mradi huo unahusisha pia ujenzi wa Jengo la Utawala, matundu 58 ya vyoo pamoja na njia ya kupanda na kushuka kwenye jengo hilo kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.