NAIBU WAZIRI PINDA KUZINDUA KLINIKI YA ARDHI MWANZA
*RC Makalla amkabidhi kitabu cha ushughulikiaji kero alioufanya katika kila Wilaya*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla leo Machi 11, 2024 amempokea Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi Mhe. Geofrey Pinda ambaye mchana wa leo atazindua Kliniki ya Ardhi kwenye Viwanja vya Nyamagana Jijini Mwanza itakayodumu kwa juma moja kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Akizungumza kwenye kikao kifupi kilichofanyika Ofisini Kwake Mkuu wa Mkoa ameipongeza Wizara ya Ardhi kwa kuamua kusikiliza wananchi hususani kwenye majiji na akabainisha kuwa Ofisi yake inaendelea na zoezi la usikilizaji kero za wananchi katika kila wilaya.
Makalla amesema katika kipindi cha mwezi Septemba na Novemba mwaka 2023 amefanya ziara katika kila wilaya Mkoani humo ambapo amewasikiliza zaidi ya wananchi 900 na kwamba asilimia 80 ya kero zilizowasilishwa kupitia mikutano yake ya hadhara zilikua ni za sekta ya ardhi hususani uwepo wa hati kinzani na madai ya fidia.
Katika kufafanua hilo Mhe. Makalla amemkabidhi Naibu waziri huyo kitabu cha kero na utatuzi wake kilichojumuisha wilaya zote ambapo ametoa wito kwa wizara kukitumua katika kufanya maamuzi yanayohusu migogo ya ardhi ambayo utatuzi ulishafanya ili kuwa na uelewa wa pamoja.
Naibu waziri Pinda ametumia wasaa huo kuipongeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kazi nzuri ya kusikiliza kero za wananchi na amemhakikishia ushirikiano na wizara yake katika kuwatumikia wananchi hususani ushughulikiaji wa haki wa kero za ardhi uliokithiri zaidi kwenye majiji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.