Mamia ya wakazi wa Ukerewe wajitokeza kuipokea meli mpya ya Mv.Butiama hapa kazi ambayo imefanyiwa marekebisho makubwa baada ya kukaa muda mrefu bila kufanya kazi .
Akizungumza wakati akiitambulisha meli hiyo kwa wananchi wa wilaya ya Ukerewe , Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amesema hizo ni juhudi za Magufuli kwani anamkakati mkubwa wa kuikomboa Ukerewe hivyo amewataka wananchi kuitumia meli hiyo kuzalisha ili kupandisha uchumi wao
"Ahadi hii ni ya Mhe. Rais Dkt. Magufuli alipokuwa anaomba kura mwaka 2015 japo kuwa hakufika huku lakini kila siku na alipokuwa anakuja Mwanza alikumbuka ahadi yake na leo amelipa deni lake hivyo visiwa 38 vitanufaika na usafiri huu "alieleza Mongella.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Mhe .Cornel Magembe alisema watu wake wamefarijika baada ya kusikia mali yao imerejea baada ya kupotea kwa muda mrefu na kuongeza kuwa wilaya hiyo ina boti mwendo kasi ambayo inatumia kubeba wagonjwa kwenda hospital ya Mwanza kwa muda wa nusu saa.
Aliongeza kuwa meli hiyo itafanya kazi siku zote bila kukumbwa na janga lolote na kupunguza muda wa wananchi kusafiri kutoka masaa manne hadi mawili pia katika eneo hilo wanazo meli kubwa mbili za serikali ambazo zinatoa huduma na kuleta mafanikio katika kisiwa hicho.
" Kuna fedha imetolewa tena na Mhe.Rais Dkt. kwa ajili ya kutengeneza abulence boti mbili hivyo kufikia Disemba mwaka huu zitakuwa zimefika eneo hilo kwa ajili ya kusaidia kubeba wagonjwa"alieleza Magembe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.