Mkuu wa wilaya ya Geita Mhe. Hashimu Komba amewataka wananchi wa mikoa ya kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi kwa lengo la kujifunza na kupata mbinu mbalimbali za kilimo, ufungaji, uvuvi na biashara katika mabanda ya maonesho ndani ya kipindi cha nane nane.
Ameyasema hayo leo agosti 3, 2025 alipokuwa akizindua na kufungua rasmi maonesho ya Saba ya nane nane kanda ya ziwa magharibi 2025 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo yanayofanyika katika Viwanja vya Nyamhongolo Ilemela-Mwanza.
Aidha, amewataka viongozi kuwa wabunifu kwa wananchi ili kuwasaidia katika kujikimu na kumudu maisha ya kila siku kwa kuwafundisha mbinu za kisasa za kisekta zinazosaidia kuongeza uzalishaj.
“Kiongozi bora ni yule aliye tayari kuja na ujuzi na ubunifu mkubwa kwa jamii ili kuweza kuleta mabadiliko chanya kwa jamii na maendeleo ya kutosha katika maeneo yake”. Amebainisha Komba.
Sambamba na hilo, ameeleza namna taifa linajengwa kwa kutegemea sekta ya kilimo na uvivu ndani ya mikoa ya kanda ya ziwa huku akibainishia kuwa zaidi ya asilimia 75 ya wananchi wanategemea kilimo, hivyo amesisitiza umuhimu wa Maonesho hayo kwa maana huwasaidia wananchi kujifunza kutokana na kuwepo kwa teknolojia zinazoleta tija.
“Wakazi wengi wa mwanza wanaishi kijiji na asilimia zaidi ya 75 wanachangia pato la taifa, wavuvi pekee wanachangia asilimia 7, mazao makuu ya biashara yamezidi kuongezeka ambayo ni pamba zao la kimkakati, migomba, mpunga na mahindi." Amesema.
Naye, Mkuu wa idara ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Mwanza Ndg. Peter Kasele amesema ongezeko la wananchi katika maonesho hayo mwaka hadi mwaka ni ishara kuwa wananchi wa kanda ya ziwa magharibi wanahamasika kuhusu kufanya shughuli za kilimo, mifugo na uvuvi kwa kuzingatia kanuni Bora na matumizii Sahihi ya teknolojia ya kisasa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.