PBZ BENKI KUFUNGUA TAWI MWANZA, RC MTANDA AMUAHIDI USHIRIKIANO
Mkurugenzi Muendeshaji wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Ndg. Arafat Ally Haji leo Septemba 04, amemtembelea ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa lengo la kujitambulisha na kuelezea mkakati wa benki hiyo kufungua tawi Mkoani humo.
Mkurugenzi Arafat amesema ujio wake huo ni sehemu ya maandalizi ya ufunguzi wa PBZ Benki hapo Mkoani Mwanza, na kwa kutambua umuhimu wa Mkoa wa Mwanza lakini pia kuendelea kuleta hamasa za kiuchumi katika Mkoa huo wameamua kusogeza huduma za kifedha kupitia benki hiyo ya PBZ.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema kitendo cha kufungua tawi Mwanza kwanza kutaimairisha muungano, pili inaashiria pia sisi Watanzania ni wamoja lakini tatu amewatoa hofu kuwa PBZ sio benki ya Wazanzibar tu bali ni benki ya wananchi wote.
Aidha RC Mtanda amesema kwa niaba ya Serikali ya Mkoa atatoa ushirikiano wa kutosha kwa benki hiyo, sambamba na hayo amewatak wasiishie mjini tu bali waende mpaka Wilayani kwani bado kuna uhitaji wa huduma hiyo ya kibenki.
PBZ Bank ni Miongoni mwa mabenki makubwa Tanzania, ikiwa na Rasilimali za Trilioni 2.05, Amana Trilioni 1.73, na Faida kabla ya kodi ya Bilioni 75.2 kwa mujibu wa hesabu za Mwaka 2023, ikiiweka benki kwenye nafasi ya 7 miongoni mwa Mabenki 44 yaliopo Tanzania
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.