PROF. MBARAWA ATAKA UPANUZI WA BANDARI YA MWANZA KASKAZINI KUHARAKISHWA
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amewataka Mamlaka ya bandari nchini kushirikiana na Mkandarasi anayejenga mradi wa upanuzi wa maboresho ya bandari ya Mwanza Kaskazini kutekeleza ujenzi huo kwa kuzingatia ubora ili thamani ya fedha ionekane.
Ametoa agizo hilo leo Januari 24, 2025 jijini Mwanza alipotembelea bandarini hapo kukagua utekelezaji wa ujenzi huo unaogharimu zaidi ya Tshs. Bilioni 18 ukihusisha upanuzi wa gati kutoka mita 98 hadi 115 pamoja na jengo la ghorofa la abiria.
Prof. Mbarawa amesema ni vema mkandarasi na wasimamizi kuzingatia uzalendo kwa Taifa kufuatia adhma ya Serikali ya uboreshaji wa gati hizo ikiwemo ya Kemondo na Bukoba ambapo kwa ujumla zitakapokamilika zitawezesha Meli kubwa ya MV Mwanza kuweza kutia nanga.
Aidha, amewataka kitengo kinachoshughulika na utengenezaji wa maboya kwa ajili ya kusaidia kutia nanga kwa meli kuharakisha na kuyaweka kwenye bandari zote ili kurahisisha utiaji nanga na kutunza meli zisipate hitilafu.
Halikadhalika, amewataka Kampuni ya Meli Tanznania (TASHICO) kukamilisha ujenzi wa Meli ya MV Mwanza inayojengwa katika bandari ya kusini kabla ya mwezi Mei mwaka huu kwani tayari upanuzi wa bandari utakua umekamilika hivyo huduma za usafirishaji zinatarajiwa kuanza.
Akihitimisha na ziara yake, Waziri Mbarawa ametembelea Kituo cha kikanda cha kuratibu, kutuatilia na Uokozi linapotokea dharula Majini kinachojengwa katika mwambao wa ziwa viktoria wilayani Ilemela na akawataka kuharakisha ukamilishaji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.