Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto yazinduliwa Mwanza
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndg. Balandya Elikana ametoa wito kwa wazazi na wadau wa watoto kushirikiana kuhakikisha kunakua na upatikanaji wa lishe bora kwa watoto ili kuwajengea afya na Siha njema ya malezi na makuzi mazuri ili kujenga Taifa imara.
Ametoa wito huo leo septemba 22, 2023 wakati akizindua Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT- MMMAM) 2021/22-2025/26 ngazi ya Mkoa katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.
"Ndugu wadau, naomba tutambue kuwa Maendeleo ya mtoto yanategemea msingi imara unaowekwa kwa malezi bora ya tangia umri wa utoto hivyo ni muhimu kuzingatia malezi bora ya watoto wetu kila siku ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa lishe bora wakati wote" Amesisitiza Ndugu Elikana.
Aidha, amesisitiza juu ya ulinzi wa watoto kuanzia kwenye ngazi za kaya kuhakikisha malezi ya watoto yanawaweka salama na kila aina ya Ukatili ili watoto wawe na makuzi bora yatakayowajengea ujasiri wa kutegemewa kuinua uchumi kwa kujihusisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Joel Mwakapala amesema kuwa programu hiyo inayokadiriwa kugharimu zaidi ya Bilioni 914.9 kutoka kwa wadau mbalimbali ilizinduliwa rasmi kitaifa na Waziri Doroth Gwajima kwa niaba ya Dkt. Samia Rais wa Tanzania kuhakikisha watoto wote tanzania kuanzia miaka 0 hadi 8 wanafikia utimilifu wao.
Aidha, amebanisha kuwa kutokana na umuhimu mkubwa wa eneo hilo programu hiyo jumuishi inashirikisha Wizara za kisekta kama Ofisi ya Waziri Mkuu eneo la Sera, Ajira, Makundi maalumu na Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu, Wizara ya Fedha pamoja na Wizara ya Mipango na uwekezaji ili kuhakikisha malengo yanatimia.
Amefafanua kuwa utafiti umefanyika kwenye maeneo ya Afya bora, Malezi yenye muitikio, ujifunzaji wa awali, ulinzi na usalama, Lishe bora na makuzi na malezi ya mtoto yenye Muitikio na ndipo imabainika katika kipindi cha umri huo ndipo ukuaji wa mtoto yanafanyika na inahitajika ukamilifu wa huduma zote ili kumhakikisha mtoto kuwa salama.
Vilevile, ametumia wasaa huo kuwasilisha ombi kwa wadau wa watoto kuhakikisha wanahusisha afua za usimamizi na uboreshaji wa watoto kwenye shughuli zao ili kuhakikisha kundi hilo linalindwa na kiendelezwa vizuri kwa ajili ya maendeleo ya Taifa la sasa na baadae.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.