RAIS SAMIA ATOA BILIONI 18 UPANUZI WA BANDARI MWANZA : RC MAKALLA
*Gati ya Kuegesha Meli kubwa ikiwemo MV Mwanza kujengwa*
*Aridhishwa na Ujenzi ataka Kasi iendane na Meli kutia nanga Mwezi Mei*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla amemshukuru Rais Samia kwa kutoa zaidi ya Bilioni 18 kwa ajili ya upanuzi wa bandari ya Mwanza Kaskazini ambao unahusisha ujenzi wa jengo la abiria pamoja na Gati kwa ajili ya Maegesho ya Meli kubwa.
Mhe. Makalla amebainisha hayo leo januari 19, 2024 alipofika kwenye Bandari hiyo kwa ajili ya Ukaguzi wa maendeleo ya shughuli hizo zinazotekelezwa chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari ya nchini.
Amesema serikali ya Rais Samia imetoa fedha hizo ili kuhakikisha sio tu upanuzi wa bandari hiyo muhimu kwa wasafiri wa ukanda wa ziwa victoria bali pia kwa ajili ya ufanisi wa uendeshaji wa Meli ya Kisasa ya MV Mwanza Hapa kazi tu ambayo inatarajiwa kukamilika mwezi Mei mwaka huu.
Makalla ameseam ameridhishwa na ujenzi wa Gati hiyo na akaagiza kasi iongezwe ili kuhakikisha mara itakapokamilika meli ya MV Mwanza iweze kupaki Bandarini hapo kwani inasubiriwa na wananchi wa ukanda wa maziwa makuu na nchi za jirani kwa ajili ya kusafirisha abiria na mizigo.
Aidha, amewataka Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuwahamishia wafanyabiashara wadogo wanaojihusisha na uuzaji wa Dagaa na Samaki kwenye eneo jingine ili wapishe ujenzi huo kwa maslahi mapana ya Taifa.
Naye, Mkurugenzi wa Halmashauri jiji la Mwanza Aron Kalugumjuli amebainisha kuwa tayari halmashauri hiyo imeandaa eneo la Nella kwa ajili ya kuwahamishia wafanyabiashara hao na kwamba kwa sasa wapo kwenye uhimarishaji wa eneo hilo kwa kuwajengea Choo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.