RAS BALANDYA AHIMIZA ULIMAJI WA KISASA WA PAMBA UWAFIKIE WAKULIMA WENGI NCHINI
Taasisi ya Utafiti wa kilimo nchini TARI na Bodi ya Pamba zimetakiwa kufanya juhudi ili utaalamu wa ulimaji wa zao la Pamba uwafikie wakulima wengi nchini tofauti na ilivyo sasa.
Akizungumza leo Julai 05, 2024 wakati wa kufunga mkutano wa Kimataifa wa kujadili utekelezaji wa mradi wa Cotton Victoria kwa upande wa Tanzania, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana amebainisha pamoja na mradi huo unaofadhiliwa na Taasisi ya Maendeleo ya ABC kutoka nchini Brazil kuonesha tija kwa wakulima lakini bado idadi kubwa haijafikiwa.
"Tuna wakulima wa Pamba hapa nchini laki sita lakini waliofikiwa na utaalamu wa ulimaji wa kisasa ni laki mbili na kumi tu, hivyo ni dhahiri bado kuna jitihada za ziada zinatakiwa kufanyika", amesisitiza Mtendaji huyo wa Mkoa wakati akitoa hotuba ya ufungaji.
Balandya amewapongeza wafadhili wa mradi huo ambao umekuwa na tija kwa wakulima kutoka kulima kwa upandaji wa awali wa sentimita 90 kwa 40 na kutoa mimea 22,222 na sasa ulimaji wa sentimita 60 kwa 30 na kutoa mimea 44,444.
"Mradi huu pia umewajengea uwezo wataalamu wetu wa kilimo wakiwemo Maafisa Ugani, TARI na Bodi ya Pamba huku wakulima wa Pamba wapatao 6522 kutoka Mwanza wakifaidika na utaalamu huo", Marco Mutunga, Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba.
Mradi wa Cotton Victoria unatekelezwa katika nchi za Tanzania,Kenya na Burundi na unamalizika mwakani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.