RAS Balandya aipongeza Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto kutoka Z'bar kwa Tafiti bora
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana leo Februari 27, 2024 amempokea na kufanya mazungumzo mafupi na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kutoka Zanzibar Abeida Abdallah na kuipongeza kwa juhudi zake kufanya utafiti mbalimbali wenye lengo la kuleta tija kwa maendeleo ya wananchi.
Katika mazungumzo hayo mtendaji huyo wa Mkoa amesema bado jamii inapaswa kuelimishwa vyema kutambua haki za watoto pamoja na wazee jambo ambalo Wizara hiyo inalifanya kwa ufanisi mkubwa.
"Nakupongeza Katibu Mkuu kwa kufika Mwanza kufunga mafunzo ya utafiti yanayolenga eneo unalo lisimamia, hizo ni juhudi ambazo zikisimamiwa vizuri zitaleta mabadiliko chanya ndani ya Jamii," Balandya
Kwa upande wake Bi Abeida amebainisha bado unahitajika mkazo wa kuelimishana na maboresho ya sheria hasa kutokana na vitendo vya ukatili kuzidi kushamiri ndani ya jamii.
"Leo tunashuhudia kuwepo na vituo vya kuwatunza wazee na watoto hii tafsiri yake watu wameshindwa kutimiza wajibu wao na kuishia kuwatelekeza," amesema Katibu Mkuu huyo wakati wa mazungumzo na mwenyeji wake.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.