*RAS Balandya aishauri Tume ya Maendeleo ya Ushirika kusimama imara kuviimarisha vyama*
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg. Balandya Elikana leo Novemba 27, 2023 amewapokea Ofisini kwake na kufanya mazungumzo mafupi na makamishna kutoka Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania na kuwashauri kuvisimamia imara vyama hivyo kwani ndiyo vyombo madhubuti vya kuinua uchumi wa mkulima na Taifa kupata pato.
Katika mazungumzo hayo Balandya amesema chama kama cha Nyanza bado kina nafasi ya kumsimamia na kumuendekeza mkulima wa zao la Pamba na mengineyo kama kitajengewa msingi imara wa namna ya kujiendesha kisasa na siyo kimazoea.
"Ujio wenu naamini mtajionea changamoto mbalimbali za chama cha Ushirikia cha Nyanza ambazo zimechangia kukiyumbisha,Serikali imeonesha nia njema ya kukipa nguvu na kujisimamia,nawaombeni muda mtakao kuwa hapa mzifanyie kazi changamoto mtakazo ziona,"amesisitiza Mtendaji huyo wa Mkoa wakati akizungumza na makamishna hao.
"Chama cha Ushirika cha Nyanza tunatambua umuhimu wake na mchango wake,hivi sasa tupo mbioni kuwa na Benki ya Ushirika naamini tutatoa elimu ya kutosha ili iwe na hisa kubwa huko,"Colins Nyakunga,Naibu Mrajisi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika.
"Ziara yetu ya siku mbili tukiwa hapa Mwanza tutahimiza sana chama hiki kiwe na wingi wa wanachama wake ambao ndiyo mtaji wa kuwa na nguvu pia kitumie vizuri fursa za mali zake kujiongezea kipato,"Richard Mayongela,Kamishna wa Tume
Ujumbe huo ambao upo Mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kujitambulisha na kuvitembelea vyama na wanachama kabla ya kuendelea na ziara yao mikoa ya Simiyu na Shinyanga.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.