RAS BALANDYA AONGOZA KIKAO CHA WATUMISHI, ASISITIZA USHIRIKIANO KUBORESHA KAZI
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana leo Disemba 28, 2023 ameongoza kikao cha watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo ambapo pamoja na mambo mengine amewapongeza kwa kazi na amewataka kuendelea kushirikiana katika kufanikisha shughuli za kila siku za kuhudumia wananchi.
Amesema katika kufanikisha hayo kila mmoja anapaswa kuhakikisha anajitoa kwa moyo wa upendo kuhudumia wananchi kwenye eneo lake na kuhakikisha aonapo changamoto anaifikisha sehemu husika kwa ajili ya kuzitatua na kuhakikisha kunakua na ufanisi kwa kufanyia maboresho kwenye eneo husika.
Balandya ameongeza kuwa katika kuhakikisha kuna usalama wa taarifa na uwasilishaji wa haraka na ufanisi wa mafaili ni lazima kutumia mfumo wa Mawasiliano wa Ofisi ambao unafikisha taarifa kwa mhusika na kwamba ofisi yake ipo kwenye mpango mahsusi wa kuboresha suala la vitendea kazi kama ununuzi wa magari ya Idara kadiri bajeti itakavyoruhusu.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi (TUGHE) tawi la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ndugu, Mangabe Mnilago amewataka watumishi kuendelea kujibidiisha kwenye kazi na Ofisi kuhakikisha wanatatua changamoto za Kimfumo ili kuhakikisha fedha zinapatikana kwa wakati na kufanikisha kusonga mbele kwa kazi.
Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Utawala na Rasilimali watu Ndugu, Daniel Machunda amewashukuru watumishi kwa kujituma na amebainisha kuwa Ofisi yake haina masuala mazito ya kinidhamu na ametumia wasaa huo kuwataka watumishi kuwahi kazini ili kuhakikisha wanatimiza malengo ya siku katika kuboresha kazi.
Katika nyakati tofauti, watumishi wamewasilisha ombi la kununuliwa Basi ili kurahisisha uendeshaji wa shughuli zinazohitaji watumishi kwenda kwenye kazi kwa makundi kwani kwa sasa Mkoa umekua ukiazima usafiri kwenye taasisi zingine mathalani Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Mei Mosi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.