RAS BALANDYA ASHAURI KUWEPO NA MPANGO WA KUTOKOMEZA UMASKINI KUEPUSHA VITENDO VYA UKATILI NDANI YA JAMII
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw. Balabdya Elikana ameshauri kuwepo na mkakati endelevu wa kuutokomeza umaskini ndani ya jamii kwa Wanawake kuwezeshwa kiuchumi hali itakayopunguza vitendo vya ukatili vinavyozidi kushamiri.
Akizungumza leo Julai 3, 2024 Ofisini kwake na ugeni kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Zanzibar ukiongozwa na Katibu Mkuu wake Bi.Zubeida Abdallah, Balandya amebainisha Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo ianze kuona umuhimu huo ambao utakuja na matokeo mazuri.
"Tukiweka mazingira mazuri kama ubora wa miundombinu kama upatikanaji wa maji na Jamii kuwezeshwa kiuchumi kwa kupatiwa mitaji ya kuboresha vipato kwenye familia vitendo vya ukatili vitapungua kama siyo kumalizika," Balandya.
Mtendaji huyo wa Mkoa ameutaka mkazo uendelee wa kuelimisha Jamii kuhusiana na vitendo vya ukatili ili watu waishi kwa amani na kuendelea na shughuli za kulijenga Taifa
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Zubeida Abdallah amesema safari yao ya kufika Mwanza ni kujifunza namna ya kupambana na hali hiyo ili Jamii iishi kwa amani.
"Kuna mradi wa tokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na watoto ulioanza mwaka huu hadi 2029, ambao huku Bara wameuanza vizuri nasi tunaamini tutapata la kujifunza." Katibu Mkuu.
Viongozi hao kutoka Zanzibar watakuwa Mkoani Mwanza kwa siku mbili wakitembelea maeneo mbalimbali yanayojishughulisha na malezi ya watu wanaoishi katika mazingira magumu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.