Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana ametoa rai kwa jeshi la polisi na waandishi wa habari kuzingatia maadili, miiko, sheria na taratibu kusimamia uchaguzi Mkuu wa 2025 uwe wa amani.
Ametoa wito huo wakati akifungua mafunzo kwa jeshi la polisi na waandishi wa habari kuhusu haki za binadamu na wajibu waakati wa uchaguzi mkuu 2025 yanayofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Balandya amesema kwa pamoja jeshi hilo na wanahabari wanalazimika kutimiza wajibu wao wa kulinda amani na kuhabarisha umma juu ya mwenendo wa uchaguzi kabla, wakati na baada ya uchaguzi katika kuelekea kuwapata viongozi.
Aidha, ametoa rai kwa makundi hayo kusimamia kampeni za wagombea nafasi mbalimbali zinazoendelea vizuri ili kuhakikisha wananchi wanasikiliza sera kwa utulivu na kujiandaa kwa uchaguzi mkuu ifikapo Oktoba 29, 2025.
Akitoa salamu kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Msataafu Mathew P. Mwaimu Bi. Saumu Mgeni ambaye ni Afisa Uchunguzi -Sheria amesema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa kwa jeshi la polisi na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria wakati wa uchaguzi.
Amesema jeshi hilo lina wajibu wa kusaidia kuzingatia haki na misingi hiyo wakati wote kwa kujiepusha na migogoro isiyo ya lazima na kuhakikisha wanalinda uhuru wa haki na amani kwa kulinda mali za wananchi.
Mafunzo hayo yanatolewa katika Mikoa 14 ya Tanzania Bara na mikoa mitano kwa upande wa Visiwani ambapo kwa upande wa mkoa wa Mwanza mafunzo yanawakutanisha washiriki 60 (Jeshi la Polisi 40 na Waandishi wa Habari 20).
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.