*RAS Balandya awataka Makatibu Muhtasi na Watunza kumbukumbu kuyatumia vyema mafunzo waliyopata Zanzibar.*
Makatibu Muhtasi na Wasaidizi wa kumbu kumbu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza waliopata fursa ya kuhudhuria kongamano la mafunzo lililofanyika kisiwani Zanzibar kuanzia Mei 23, 2023 hadi Mei 27, 2023 Wameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kuwapatia fursa ya kuhudhuria kongamano hilo wote kwa pamoja.
Shukran hizo wamezitoa leo kwa Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndg Balandya Elikana kwa kuwapa nafasi hiyo kwa pamoja na kuahidi kuyatumia vizuri mafunzo hayo ili kuongeza tija katika kazi zao za kila siku.
"Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itaendelea kuwapa nafasi hizo kila mwaka kwani unatambua umuhimu wake na nawasihi kuendelea kuchapa kazi kwa bidii mkizingatia miongozo yenu",amesisitiza Balandya
Aidha Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndg Daniel Machunda amewashukuru watumishi hao kupata mafunzo hayo na kuwaahidi Ofisi yake kuwapa ushirikiano ili majukumu yao ya kazi wayafanye kwa kuzingatia Weledi.
"Kongamano lenu linafanyika kila mwaka,mwakani bajeti ikiruhusu tutahakikisha mnahudhuria kwa wingi ili muongezewe ujuzi zaidi katika kazi zenu",Machunda
Jumla ya watumishi 11 kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wamehudhuria kongamano hilo la mafunzo kisiwani Zanzibar
Kongamano la Mafunzo la TAPSEA mwakani litafanyika Mkoani Mwanza kuanzia Mei kabla ya mwaka 2025 kufanyika kisiwani Pemba.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.