Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza,Ngusa Samike amefanya ziara ya ukaguzi wa Dawa na Vifaa Tiba Vituo vya Afya Wilayani Sengerema na kuagiza Vituo vyote vya Afya viwe na huduma ya watoto chini ya miaka 5 wenye upungufu wa hewa ya Oxygen mwilini.
Katibu Tawala Ngusa akiwa katika Kituo cha Afya Kamanga Wilayani Sengerema amepata taarifa ya huduma hiyo ijulikanayo kitaalam kama TIMCI ambayo ipo kwenye Utafiti hadi mwaka 2024 inatolewa kwenye Vituo 23 Wilayani humo.
"Hii ni huduma muhimu sana watoto wengi wanapozaliwa wanapitia katika changamoto mbalimbali ambazo bila uangalizi wa kitaalam wanapoteza maisha,tufanye jitihada za haraka isambae Wilaya zote za Mkoa wa Mwanza"
Mratibu wa Huduma hiyo inayotibu changamoto zote za upumuaji kwa mtoto Dktr Mujungu Deusdedit amesema mara baada ya Utafiti huo kumalizika watalifanyia kazi agizo la Katibu Tawala kutokana na umuhimu wa Huduma hiyo kutolewa sehemu zote.
Kwa mujibu wa Takwimu hadi mwezi huu jumla ya watoto 6224 wamepimwa wingi wa Oxygen mwilini na 80 wamekutwa na upungufu huo na kupatiwa matibabu na kunusuru maisha yao.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dktr Thomas Rutachunzibwa amesema wanaendelea kuboresha huduma za afya kwenye Vituo na sasa mkazo wameweka upande wa vifaa vya upasuaji.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Dktr Saumu Kumbisaga amebainisha Hospitali ya Wilaya ipo katika hatua za mwisho kuanza kutoa huduma kwa Wananchi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike ametoa agizo Wilayani Sengerema Miradi yote ikamilike kwa wakati, kuwepo na utaratibu sahihi wa matumizi ya dawa na Vituo vya Afya visikae na makusanyo ya pesa na badala yake zipelekwe bank.
Wilaya ya Sengerema ina jumla ya Vituo vya Afya 46 vinavyomilikiwa na Serikali Zahanati 41 na Vituo 5.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.