Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike ameendelea na ziara ya ukaguzi wa Dawa na Vifaa Tiba Sekta ya Afya,akiwa Wilayani Magu amehimiza Hospitali na Vituo vya Afya kuzingatia matumizi sahihi ya dawa ili kuiepusha Serikali hasara ya dawa hizo kuchina.
Akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Magu,Katibu Tawala Ngusa amesema ni lazima kuwepo na taarifa sahihi wakati wa kuagiza.
dawa au kutambua mapema ni kituo gani cha Afya kina upungufu na kufanya uamuzi sahihi.
"Nawakumbusheni tena maana ziara zangu nahimiza hili jambo tangulizeni uwajibikaji bora na siyo mkae tu ofisini na kuletewa taarifa hapo mtaharibu kazi"
Aidha ameipongeza Hospitali ya Wilaya ya Magu kwa kuweka takwimu sahihi na kuwafuatilia tiba zao Waathirika wa VVU hali ambayo amesema inasaidia kupunguza maambukizi.
Kuhusu tatizo la Fistula Ngusa ameitaka jamii kutowanyanyapaa watu wenye hali hiyo na badala yake kuhimizana kwenda kupata huduma Hospitali kwani tatizo hilo linatibika
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dktr Thomas Rutachunzibwa amesema marafiki wa Maendeleo kama Asasi isiyo ya Kiserikali ya AMREF wamekuwa wakisaidia kutoa elimu na gharama za matibabu ya magonjwa mbalimbali maeneo ya Vijijini.
Katika ziara hiyo Wilayani Magu,Katibu Tawala Ngusa pia amevitaka Vituo vyote vya Afya vilivyokamilika ujenzi kwa asilimia 80 vianze kutoa huduma kwa Wananchi.
Wilaya ya Magu ina jumla ya Vituo 51 vya afya vikiwemo 44 vya Serikali,taasisi za kidini na watu binafsi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.