Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike ameendelea na ziara ya ukaguzi Sekta ya Afya Wilaya za Mkoa huo, akiwa Wilayani Ukerewe amewataka Waganga Wakuu wa Wilaya kuongeza umakini katika majukumu yao.
Katibu Tawala Samike akiwa Kisiwa cha Ilugwa Wilayani Ukerewe amesema amebaini tatizo la uagizaji dawa kiholela,kutokuwepo na kumbukumbu sahihi za matumizi ya dawa na kuchina kwa dawa kutokana na kukaa muda mrefu bila kutumika.
"Waganga Wakuu nawaambia katika hili sitakuwa na huruma hatua za kinidhamu ni lazima zitachukuliwa haiwezekani Serikali ipate hasara na wahusika mpo"
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dktr Thomas Rutachunzibwa amesema maelekezo yote ya Katibu Tawala wameyapokea na kuyafanyia kazi.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Dktr Getera Nyange amesema changamoto zote zilizobainika wamejipanga kuzitatua kwa kuwajengea uwezo baadhi ya Watumishi husika.
Kuhusu Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto, ameikumbusha Jamii kushikamana ili kuitokomeza hali hiyo kwani wingi wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu umechangiwa na kupotea kwa msingi imara wa malezi.
Aidha Katibu Tawala Ngusa Samike amewakumbusha Wakandarasi wanaoendelea na Miradi ya ujenzi ya Vituo vya Afya kuzingatia suala la Mazingira kwa kutokata Miti.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.