Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike amezitaka Halmashauri zote Mkoani humo kukamilisha Miradi yote ya Vituo vya Afya na mfumo wa upokeaji na ugawaji wa dawa uwe sahihi.
Katibu Tawala huyo akiwa Wilayani Kwimba katika ukaguzi wa Miradi hiyo amesema amejionea Vituo vya Afya vikiwa vimekamilika lakini huduma bado wakati Wananchi wanatembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.
"Mfumo wa upokeaji na kutoa dawa nao nimeona una tatizo nimeingia Stoo za utunzaji napo nimegundua watu wanafanya kazi kimazoea tu hii siyo sahihi" amesisitiza Ngusa Samike.
Amewataka Viongozi wa Halmashauri Kaimu Mkurugenzi Dennis Kabogo na Mganga Mkuu wa Wilaya,Elias Misana kumpa taarifa ya Maendeleo kila wiki ili aone hatua za mabadiliko waliyofanya.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Thomas Rutachunzibwa amesema msongamano wa Wananchi Hospitali za mijini sasa umepata ufumbuzi kutokana na huduma hiyo kuwasogelea Wananchi kutokana na Wilaya zote za Mkoa wa Mwanza kuwa na Vituo vingi vya Afya.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kwimba,Elias Misana amesema changamoto zote zilizobainika katika ziara ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza wanazifanyia kazi hasa eneo la mfumo wa dawa.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike anafanya ziara Wilaya zote za Mkoa huo akikagua Miradi ya Maendeleo Sekta ya Afya pamoja na Huduma zitolewazo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.