Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana, ameongoza waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa mtumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Celestine Mahubi.

Mazishi hayo yamefanyika leo tarehe 14 Novemba 2025 katika Kijiji cha Kanoni (Maisome) Kata ya KahundaTarafa ya Nyehunge Wilaya ya Sengerema ambapo mamia ya ndugu, jamaa, watumishi wenzake na viongozi mbalimbali wamejitokeza kumpa heshima ya mwisho.

Bw. Elikana akitoa salamu za pole amesema kuwa marehemu Mahubi atakumbukwa kwa uadilifu weledi na mchango wake mkubwa katika masuala ya upatikanaji wa majisafi na usafi wa mazingira mkoani Mwanza.

‘’Naitakia familia faraja, akisisitiza kuwa serikali inatambua kazi na alama aliyoiacha marehemu katika sekta ya maji”.

Mungu aiweke roho yake mahali pema.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.