RAS MWANZA APONGEZWA UENDESHAJI MAKINI WA BARAZA LA WAFANYAKAZI
Mwenyekiti wa TUGHE Taifa Ndugu Joel Kaminyonge amempongeza Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bwana Balandya Elikana ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kusimamia vema Baraza la ofisi hiyo ikiwemo kufanya vikao vya kisheria kwa wakati pamoja na kupeleka watumishi kwenye mafunzo mbalimbali yanayoandaliwa na TUGHE.
Ametoa pongezi hizo mapema leo Jumatano tarehe 12 Machi, 2025 wakati akisalimia wajumbe wa baraza hilo kwenye Ukumbi wa Rock City Mall ambapo baraza hilo linakutana kwa ajili ya kikao cha kawaida cha kikanuni ambapo pamoja na mambo mengine wajumbe watafanya uchaguzi wa Katibu na Katibu Msaidizi pamoja na kupitisha bajeti kwa mwaka 2025/26 kwa ofisi hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.