Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg.Balandya Elikana amewakumbusha walimu walezi na Wazazi kuzingatia na kuyafanyia kazi mafunzo mbalimbali wanayopatiwa ili yawe na tija kwa Taifa.
Akifungua leo Jijini Mwanza Mafunzo ya kukabliliana na unyanyasaji wa kijinsia na majanga ya moto kwa walimu walezi kutoka Shule za msingi Jijini Mwanza Katibu Tawala msaidizi Uchumi na Uzalishaji Emil Kasagara aliyemuwakilisha Katibu Tawala amesema bado kunahitajika umakini katika malezi ya wanafunzi shuleni kutokana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kuendelea kushamiri nchini.
"Niwapongeze Taasisi ya Elimu ya Watu wazima kwa kutoa mafunzo haya ambayo yana lengo jema kwa Taifa letu,wajibu wetu sasa tuhakikishe yaje na matokeo chanya kwa kutokomeza vitendo vya unyanyasaji kwa watoto wetu"amesisitiza Katibu Tawala msaidizi.
Ameishauri pia Taasisi ya Elimu ya Watu wazima kuangalia namna ya utoaji wa mafunzo kama hayo kwa makondakta wa mabasi ya abiria na madereva wa bodaboda ambapo kumekuwa na tabia za unyanyasaji kwa baadhi yao.
"Tumejipanga kuona baada ya mafunzo haya kuna hatua gani za mabadiliko,ofisi yangu kwa kushirikiana na Viongozi wenzangu tutaendelea kufuatilia ili lengo letu la kujenga Taifa lililostaarabika litimie" Maenda Chambuko Afisa Elimu Watu wazima Mkoa.
"Ukimuelimisha Mwalimu tambua umewaelimisha watu mia moja nyuma yake,nimefarijika na mafunzo haya naamini walimu ambao muda mwingi mnakaa na watoto wetu mtakwenda kuwa muarobaini wa changamoto hii ya unyanyasaji"Mhe Diwani.Magreth Kuhanwa,Mwenyekiti Huduma za Jamii Baraza la Madiwani Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
"Majanga ya moto yameigharimu sana Serikali kutokana na baadhi ya shule zake kuteketea kwa moto,kupitia mafunzo haya washiriki muwe makini kuwasikiliza Wataalamu kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili muwe na ujasiri wa kupambana na majanga ya moto yanapotokea"Dkt.Beatus Mwendwa Mkuu wa Chuo Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kituo cha Mwanza.
Mafunzo hayo ya siku moja yamewashiriksha Walimu walezi 146 kutoka Shule za Msingi Wilaya ya Nyamagana.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.