Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza,Balandya Elikana leo ameupokea ugeni kutoka Serikali ya Malawi ukiongozwa na Naibu Waziri wa Afya Enock Phale ambao upo nchini kwa ziara ya kujifunza mifumo ya Afya.
Akizungumza na ugeni huo uliomtembelea ofisini kwake, Bw Balandya amesema ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Malawi umezidi kuimarika kwa kushirikiana kwenye nyanja mbalimbali.
"Ujio huu wa Naibu Waziri wa Afya kutoka Malawi pamoja na ujumbe wake utakuwa na faida kwa pande zote mbili kwani hata sisi lipo la kujifunza kutoka kwao huu ndiyo uhusiano bora" amesema Katibu Tawala
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya kutoka Malawi Mhe Enock Phale amesema Tanzania imepiga hatua katika Sekta ya Afya hasa katika magonjwa ya moyo ambayo awali kulikuwa na idadi kubwa ya wanaokwenda kutibiwa nje tofauti na sasa wanapata huduma hiyo hapa nchini,tunaamini kuja kwetu tutajifunza mengi.
Naye Naibu Waziri wa Afya Mhe.Dkt Godwin Mollel amesema ugeni huo umetembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete,Hospitali ya Mwananyamala pamoja na Bugando lengo likiwa kujifunza mifumo mbalimbali inavyofanya kazi.
Ujumbe huo kutoka Malawi umeambatana na baadhi ya madaktari na Wataalam wa Tehama.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.