RAS Mwanza awataka Watumishi wa Umma kusimamia weledi Utekelezaji mradi wa FIKIA
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Daniel Machunda amewataka watumishi wa umma wanaohusika katika utekelezaji wa mradi wa FIKIA PLUS kufanya kazi kwa bidii na weledi na kuhakikisha wanafikia asilimia 100 za matumizi ya fedha za mradi zilizotengwa katika bajeti.
Ametoa maagizo hayo leo wilayani Misungwi kwenye kikao kazi cha siku 2 cha tathmini na maandalizi ya mpango kazi na bajeti mpya ya Mradi wa FIKIA PLUS unafadhiliwa na Shirika la ICAP kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Gwambina Hoteli.
Amesema, Mkoa umewahaikishia Wafadhili yaani ICAP na CDC kuwa utatoa ushirikiano katika utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha unatekelezwa kwa viwango vya juu na amewapongeza ICAP kwa kuwa na ushirikishaji katika maandalizi ya bajeti ya mradi huo.
Amebainisha kuwa kwa kipindi cha miaka 2 iliyopita ya mradi kama mkoa hatukuweza kuwa na matumizi ya fedha kwa asilimia 100 jambo ambalo siyo sawa kutokana na kuwepo kwa mahitaji makubwa katika kufikia malengo ya kupambana na kuthibiti maambukizi ya Ukimwi kwenye Jamii.
Aidha, Machunda amefafanua kuwa
mwaka wa fedha wa mradi huo unaaanza Oktoba 2023 na kuisha Septemba 2024 na kwamba kikao hicho kimefanya tathmini ya utekelezaji wa mradi kwa mwaka 2022/2023 na kuandaa mpango kazi na bajeti ya 2023/2024.
Mkoa wa Mwanza umejipanga kuendelea na mapambano dhidi ya UKIMWI na udhibiti wa maambukizi mapya ili kufikia lengo la kitaifa la kuwa na maambukizi mpya sifuri ifikapo 2030.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.