RC MAKALLA AAGIZA UONGOZI JIJI LA MWANZA UREJESHAJI WAFANYABIASHARA SOKO KUU MWANZA UWE WA WAZI
*Ataka Utaratibu wa kurejesha kuanza na wafanyabiashara walioondolewa awali*
*Asema hakuna Kizimba kulichotolewa kwa mfanyabiashara hadi sasa*
*Asema Mkandarasi atalipwa fedha baki wiki ijayo*
*Amshukuru Rais Samia kutoa fedha za Ujenzi wa Soko hilo*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla amewaagiza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuhakikisha Ugawaji wa Vizimba kwenye Soko Kuu la Mjini Kati mara litakapokamilika unakua wa Uwazi na wenye ushirikishaji wa Makundi ya Wafanyabiashara wenyewe.
Makalla ametoa agizo hilo leo tarehe 19 Januari 2024 wakati alipofika kwenye Soko hilo kukagua Maendeleo ya Ujenzi wake unaogharimu zaidi ya Bilioni 25 na kubaini kuwa wapo kwenye hatua za Ukamilishaji kwani wamefikia asilimia 93 ya ujenzi.
"Hili ndilo soko haswa lenye hadhi ya Jiji na Mkoa wa Mwanza, tunamshukuru sana Mhe. Rais kwa kutoa fedha za Ujenzi wa Soko lenye uwezo wa kubeba wafanyabiashara zaidi ya 1400 tofauti na 400 walioondolewa siku za nyuma kwenye soko hilo." Makalla.
Makalla amewatoa hofu wananchi wanaodhani kwamba tayari vizimba vimeanza kugawiwa kwenye eneo hilo na akatoa tamko kuwa hakuna hata kizimba kimoja ambacho kimetolewa kwa mfanyabiashara na kwamba watapewa kipaumbele walioondolewa kwenye soko la zamani.
Vilevile, amebainisha kuwa wiki ijayo Mkandarasi atalipwa Bilioni 1.3 zilizobaki kwenye mradi huo hivyo anapaswa kuongeza spidi ya ujenzi ili mwezi Machi amalize ujenzi na kukabidhi Soko hilo ili wafanyabiashara warejeshwe na wengine wanufaike nalo.
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Mhe. Sima Costantine amebainisha kuwa kupitia Bilioni 2 zilizotengwa kwa ajili ya Miundombinu zitasaidia kuweka sawa kwenye uhimarishaji wa barabara ya kuingia kwenye Soko hilo ili wafanyabiashara wapate urahisi kwenye shughuli zao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.