RC Makalla agawa Pikipiki 46 kwa Maafisa Ugani-Mifugo kutoka Halmashauri 8 za Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla leo amegawa Pikipiki 46 kwa Maafisa Ugani-Mifugo kutoka Halmashauri 8 za mkoa huo na kuwataka kwenda kuzitumia kwa makusudi yaiiyolengwa na siyo vinginevyo nevyo.
Akizungumza kwa niaba yake kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakati wa hafla fupi ya makabudhiano hayo, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi,Mhe. Paul Chacha amebainisha Serikali inaendelea kuiboresha sekta ya Mifugo kwa kuweka mazingira rafiki kwa Maafisa hao, hivyo nao ni wajibu wao kuhakikisha wanakuwa chachu ya mageuzi chanya kwenye sekta hiyo.
"Hizi Pilipiki siyo muende kuzigeuza bodaboda na kujipatia kipato hapo mtakuwa mnakosea na hatua za kinidhamu zitachukuliwa, nendeni muwafuate wakulima walipo na mkstoe elimu ya kutosha," Mhe.Chacha
Amewataka pia Wakurugenzi wote wa Halmashauri kuhakikisha wanawapatia mafuta ya kutosha ili wasikwame katika shughuli zao za kila siku.
Kwa upande wake Katibu Tawala msaidizi uchumi na Uzalishaji,Emil Kasagara amesema Plkipiki hizo zimekuja wakati mwafaka kutokana na kuwepo na mradi wa kunenepesha ng'ombe na kituo atamizi kwenye shamba la Taifa la mifugo Mabuki.
"Mhe.Mkuu wa Wilaya hapo Mabuki Serikali imepeleka ng'ombe 500 kwa ajira ya mradi wa unenepeshaji na kuna vijana 90 wanapata mafunzo hayo,hivyo maafisa Ugani hawa wamerahisishiwa kazi ya kwenda kusaidia kutoa elimu,"
"Tunaishukuru Serikali ya Rais Samia kwa kutuwezesha nyenzo hizi,siku za nyuma tulipata wakati mgumu katika kutimiza majukumu yetu",Arsen Mwenda,Afisa Ugani-Mifugo Kwimba.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.