RC MAKALLA AHIMIZA KUHARAKISHWA MAENDELEO YA WANANCHI MAGU
*Aagiza miradi ya maendeleo ikamilike kwa wakati, ubora na ilingane na thamani ya fedha*
*Ataka iwepo ratiba maalum ya ufuatiliaji wa Miradi*
*Aipongeza Halmashauri ya Magu kwa kuwa na hoja chache*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA. Amos Makalla ameitaka Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu kuisimamia miradi ya maendeleo ili kutimiza matarajio ya wananchi.
Mhe. CPA. Makalla amesema hayo leo Juni 27, 2023 wakati wa Mkutano wake wa mwisho wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu kwa ajili ya kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) za Mwaka 2021/22 zinazoishi Tarehe 30 Juni 2022.
" Tukasimamie miradi ya maendeleo ibadilike kutokukamilika kwa miradi hiyo tunafifisha imani ya wananchi tutumie matarajio ya wananchi kama tulivyo ahidi kuhakikisha inakamilika kwa kiwango kinachotakiwa kwa thamani ya fedha kwa kufanya hivyo tutaendelea kuwatendea haki wananchi wetu," RC Makalla.
"Wekeni ratiba ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa menejimenti tekelezeni yale ambayo yanaelekezwa katika ilani Chama cha Mapinduzi CCM, Madiwani wamekamilisha wajibu wao ni kazi ya menejimenti yale mliyoyaahidi katika vikao vya kujibu hoja kuyatekeleza kila mmoja katika eneo lake.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa ameitaka Halmashauri hiyo kuendelea kutoa ushirikiano kwa ofisi ya CAG katika kila hatua ili ukaguzi ujao kusiwe na hoja pia kumtumia vizuri mkaguzi wa ndani katika kuhakikisha wanazimaliza hoja.
Vilevile RC. Makalla ametoa rai kwa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Kufanyia kazi taarifa za mkaguzi wa ndani ili kupunguza hoja na Menejimenti kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wakaguzi ili waweze kupata hati safi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mhe. Mpandalume Simon amesema wanakwenda kutufanyia kazi mpango kazi ambao utaenda kujibu hoja zote za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Naye, Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Mkoa wa Mwanza Waziri Shabani kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amesema anatambua ushirikiano alioupata kutoka kwa wafanyakazi na menejimenti ya Halmashauri ya wilaya ya magu wakati wa ukaguzi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.