RC MAKALLA AIPONGEZA BENKI YA NMB KUWA TASISI KINARA KULIPA KODI NCHINI
*Aipongeza Bodi ya Wakurugenzi, Mkurugenzi mtendaji,Menejimenti na Watumishi kwa Ushirikiano*
*Awakaribisha Benki ya NMB kusaidia wawekezaji kuwekeza kwenye Utalii Mwanza*
*Awasihi kuendelea kubuni bidhaa rafiki kwa makundi mbalimbali hususani walimu*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla ameipongeza Benki ya NMB kwa kuwa mlipa kodi mkubwa na bora zaidi 2023 na kupata tuzo Novemba 24, 2023 .
Ametoa pongezi hizo mapema leo Novemba 30, 2023 alipokua akihutubia mkutano wa Mameneja wa Benki hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Malaika- Mwanza.
Makalla amesema mafanikio yoyote yanatokana na uongozi bora na ushirikiano hivyo bodi ya wakurugenzi, menejimenti na watumishi wamefanya kazi nzuri sana iliyozaa matunda hayo.
Aidha, amesema pamoja na kuongeza kuchangia pato la Taifa, hawana budi kuendelea kubuni bidhaa bora na rafiki kwa makundi mbalimbali ili kusaidia wananchi hususani kwenye huduma za mikopo.
Akizungumzia tuzo waliyopata ya kuwa taasisi inayolipa kodi kubwa zaidi tena kwa hiyari, Makalla amewasihi kuendelea hivyo kwani wanakua ndio chachu ya uboreshaji wa huduma za kijamii kama maji, miundombinu ya barabara, kilimo, afya na elimu.
Awali Mkuu wa Idara ya wateja wa Benki hiyo, Aikansia Muro alibainisha kuwa juma lililopita Benki hiyo ilipata Tuzo ya Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ya kuwa mlipa kodi mkubwa na bora zaidi, Taasisi inayolipa kodi kubwa zaidi pamoja na walipa kodi bora kwa hiyari.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.