RC MAKALLA AKEMEA HUJUMA KWENYE MIRADI INAYOTEKELEZWA MWANZA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA Amos Makalla amesema hatokuwa tayari kuona baadhi ya watu wanazorotesha miradi mbalimbali inayotekelezwa Mkoani humo na badala yake hatua kali za kisheria watachukuliwa.
Akizungumza leo kwa niaba yake wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa mikataba miwili ya ujenzi wa Tanki la maji Nyamazugo na upanuzi wa mtandao wa bomba Km 73 Wilayani Sengerema,Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza,Ndg.Balandya Elikana amesema wananchi wanapaswa kutanguliza uzalendo kwa kuilinda miradi hiyo kwani ipo kwa faida yao.
"Hizi hujuma hatuwezi kuzifumbia macho,miradi inaletwa kwetu ili irahisishe maendeleo,unapofanyika wizi ni dhahiri miradi hiyo haiwezi kumalizika kwa wakati na hatimaye malengo yaliyo kusudiwa kushindwa kumalizika kwa wakati,"amesisitiza Mtendaji huyo wa Mkoa.
Amesema mradi anaoshuhudia ukitiwa saini tayari kwa ujenzi wa Tanki la maji la ujazo wa lita 5,000,000 wenye thamani ya Shs bilioni 2.7 na upanuzi wa mtandao wa bomba wa Km 73 wa thamani ya Shs milioni 937,673,750,hizo ni fedha nyingi zinazotolewa na Serikali kwa kuthamini maendeleo ya wananchi hivyo ni wajibu kwa kila mmoja kuunga mkono jitihada hizo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Sengerema,Mhe.Senyi Ngaga amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu kwa kuonesha kwa vitendo jitihada za kuwaletea maendeleo wananchi kwa miradi mbalimbali kuanzia sekta ya afya,elimu,na maji.
"Nina kila sababu ya kuishukuru Serikali hii ya awamu ya sita kwa hizi jitihada za kumtua mama ndoo kichwani,kwa miaka ya nyuma wananchi wangu wa Jimbo la Sengerema wametaabika sana na upatikanaji wa huduma hii ya maji,"Mhe Hamis Tabasamu,Mbunge wa Sengerema CCM
"Mradi huu wa Tanki la maji utakapo kamilika utaweza kuhudumia wakazi wa Sengerema wapatao 166,500 hivyo kuzidi kwenda na malengo ya Serikali ya kufikisha huduma ya maji kwa asilimia 95 mjini na asilimia 85 vijijini ifikapo mwaka 2025,"Mhandisi Sadala Hamisi,Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Sengerema(SEUWASA)
Mradi wa ujenzi wa Tanki la maji utatekelwzwa na Mkandarasi NANGH'WARE MHANDI LIMITEDH na ule wa upanuzi wa mtandao wa bomba Km 73 wakandarasi ni 3 Zabuni ya bomba ni LAKE PIPES LIMITED,Zabuni ya viungio vya mabomba ni KAKENGI INDUSTRY AND GENERAL SUPPLY na Zabuni ya uchimbaji muhusika ni LOCAL FUNDI.
Miradi hiyo itatekelezwa kwa muda wa miezi 6 kuanzia Agosti mwaka huu hadi January 2024.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.