RC MAKALLA AKIPONGEZA KIWANDA CHA UCHENJUAJI NA USAFISHAJI WA MADINI
*Aridhishwa na Biashara ya Madini katika Soko la Madini Mwanza*
*Aahidi Mkutano mkubwa wa wadau wa Madini*
*Asema Mgodi mkubwa wa Pili Tanzania wa Nyanzaga kuanza Mwezi septemba wilayani Sengerema*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA Amos Makalla amekipongeza kiwanda cha uchenjuwaji na usafishaji madini kwa kufanya shughuli zake kwa Teknolojia ya juu hali inayofanya dhahabu ya kutoka Tanzania kuwa na viwango bora kwenye soko la Dunia.
Akizungumza leo na wanunuzi wa madini na uongozi wa kiwanda cha kusafisha madini wakati wa ziara fupi aliyoifanya kiwanda hapo Wilayani Ilemela, Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha thamani ya uwekezaji huo wa Bilioni 16.5 umekwenda pamoja na ubora wa shughuli husika na Serikali kuwa na uhakika wa mapato.
"Nimefika hapa nimejionea kazi zinavyofanyika na taarifa za kiwanda hiki hakika nawapa pongezi,nitawatembelea wachimbaji Kwimba na Misungwi kuwapa hii taarifa namna Serikali ilivyoweka mazingira mazuri kwao na waitumie fursa hii ",CPA Makalla.
Aidha, Mhe. Makalla ameridhishwa na biashara ya madini katika soko la bidhaa hiyo mara baada ya kuwasikiliza na kujionea shughuli zao na kuwaahidi Serikali ya Mkoa kuwasaidia kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili ili wafanye shughuli zao katika mazingira rafiki na kuendelea kuwawekea mazingira mazuri wawekezaji watakaojitikeza.
"Nimezungumza na Afisa Madini wa Mkoa Mhandisi Nyaisara Mgaya aandae taarifa zote muhimu kuhusiana na shughuli za Madini ili wadau wapate ufahamu wa kutosha wakati wa mkutano mkubwa nitakao itisha",amesisitiza Makalla.
"Nimezungumza na mwekezaji wa mgodi wa Nyanzaga wenye thamani ya Dola milioni 474 ambao utaanza shughuli zake hivi karibuni,watumie kikamilifu fursa zilizopo kiwandani hapa na siyo kwenda sehemu nyingine Mhe.Makalla
"Kiwanda hiki mhe.Mkuu wa Mkoa kina mitambo ya kisasa ya kusafisha madini na kuifanya kuwa kwenye ubora wa kimataifa na hivi sasa tunatarajia Benki Kuu ya Tanzania kuja kuyanunua Madini hapa kama sheria inavyoelekeza,"Deus Magala,Meneja Rasilimali Watu Kampuni ya Uchimbaji Madini,STAMICO.
"Mhe.Mkuu wa Mkoa sisi kama wadau wa Madini Bado tuna changamoto za hapa na pale hasa upungufu wa malighafi ambao unatufanya tutumie muda mwingi kusubiri na wakati mwingine kutufanya kutoka na kwenda sehemu nyingine kutafuta Madini,"William Kulindwa,Mwenyekiti soko la madini Mwanza.
Kiwanda cha kusafisha madini kilichoanza shughuli zake mwaka 2021 baada ya kuzinduliwa na Rais Dkt.Samia Suluhu,kinafanya kazi kwa ubia kati ya Serikali yenye asilimia 25 na mwekezaji kutoka Sudan mwenye asilimia 75
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.